Wednesday, February 01, 2006

Kasi ya Ujambazi: Kinga ni bora kuliko tiba.

Mrema aulizwe alifanikiwaje kwa hili?

Kumekuwa na gumzo kutoka kila pembe ya nchi hii iitwayo ya amani na utulivu juu ya kuzidi kwa wimbi la ujambazi karibia nchi nzima.

Majambazi na ujambazi kwa vyovyote na kwa hali yeyote ile huleta athari ambazo ni kunyume na neno la Amani na utulivu katika jamii yeyote ile. Na kwamba ujambazi wa kuvamia sehemu mbalimbali nchini umepamba moto na badom unaendelea kutishia amani ya wananchi aidha wawapo kwenye kumbin za starehe, majumbani wamejipumzisha baada ya kazi zao za siku za kihalali, sokoni, madukani wakifanya shopping zao kama kariakoo na kwingineko. Kupamba moto huku kwa majambazi kulikuja tu baada ya serikali ya awamu ya nne kutangazwa na kuundwa wizara mahususi ya kupambana na uhalifu nchini, wizara ya Usalama wa raia chini ya waziri Kharith Bakari Mwapachu.

Hata hivyo, yamesemwa mengi na wanacnhi juu na kuhusu kilio, mapendekezo juu ya kukithiri kwa ujambazi au uhalifu wa majambazi nchini.
Kwangu binafsi sihitaji kuyarudia yoote yale ambayo yameshasemwa na waliotangulia wananchi wenzangu kwa serikali, lakini labda nizidi tu kuongezea pale paliposahaulika au kama wazo mbadala kwa serikali ya wana ari, nguvu na Kasi mpya juu ya kulidhibiti janga hili la ujambazi kwa watanzania wasio na hatia na wanaojitafutia ridhiki zao kiuhalali.

Napenda na kwa mapenzi yote ya nchi yangu na watu wake, naishauri serikali ya awamu ya nne chini ya wizara ya usalama wa raia kwamba kama ujambazi na majambazi yanashindikana kudhibitiwa na vitendo vyao, Basi serikali haina budi na isione aibu yeyote kumuuliza Mheshimiwa(kwangu) Agustino L.Mrema, Mwenyekiti wa chama cha TLP, ni kwa jinsi gani?, njia zipi? Na kwa vipi yeye binafsi alikuwa akizitumia na kuweza kudhibiti na kupunguza wimbi la ujambazi na athari zake twaweza kusema ni kwa zaidi ya asilimia 80 alipokuwa waziri wa mambo ya ndani?.

Hili kwa mtanzania yeyote ni shahidi kwa serikali ya awamu ya pili Mrema alipoagiza majambazi sugu na silaha zao kuzisalimisha kituo cha polisi chochote nchini kabla ya wao hawajatiwa mikononi mwa serikali. Wala hatujasahu hilo na hakuna asiyefahamu na kwa hilo Mrema nampongeza. Kwa mantiki hiyo juhudi za Mrema kwa jambo hili waweza kuzilinganishaje na juhudi za sasa katika ujambazi pamoja na kuwepo wizara maalum ya kushughulikia suala kama hili?, au ndo imekuwa kama wametria petroli kwenye moto unaowaka kuuongezea?. Hali inazidi kutisha, wananchi wanauawa, mali zao zinapokonywa na kurudishwa kwenye umaskini huu huu tunaoupigania kuuondoa kwa kutumia MKUKUTA unakuwa kikwazo kwa Ujambazi.

Isitoshe, kama mheshimiwa rais aliposema baada ya kuapishwa uwanja wa taifa, aliwaambia wana-CCM kuwa wasiwabeze sana wapinzani kwani hata wao wapo waliowapa kura na sasa hatuna budi kuacha kugombana na kuanza kuzima moto unaoteketeza nyumba yetu. Na hivyo ndivyo hivyo, mamuomba Mheshimiwa Mrema kwa kuzingatia busara zake na busara ya Mheshimiwa rasi aliyoisema basi atakapoitwa asisite kuwasaidi watanzai mikakati aliyoitumia kudhibiti ujambazi.

Na wewe mheshimiwa Mwapachu nakuomba kwa niaba ya wananchi wenzagu acha kuficha maradhi, kifo kitakuumbua, anika matatizo yako ya ujambazi kwa A.L.Mrema upate fimbo na dawa kwa wizara yako inayoonekana ni ngumu, na kweli ngumu kwa hali inavyotisha sasa.Bwana Mrema kwa imani yangu anatupenda wanachi wake na ana uchungu na nchi yake, na ndo maana huwa yupo kutetea kwa lolote kama serikali haitendi yaliyo haki na kwa mantiki hiyo tunaomba kwa pande zote make mjadiliane.Jamni si tunajenga nyumba moja, basimtusaidiane huyu kuleta bati, huyu ufito, huyu mfuko wa simentio ili mradi nyumba bora ikamilike,Mrema saidia , Mwapachu kaa na huyu mheshimiwa muulize atakusaidia tuu.

Nafikiri hapatakuwa na aibu yeyote kwa serikali yetu kupata njia mbadala kutoka kwa watu mbalimbali na si kauli za kuua muwapatapo majambazi.je chanzo chake mnacho?,dalili zake je?, mmh! Yangu macho.

"Kwa ukweli huu sitakuwa adui kwa serikali yangu ."

5 Comments:

At 9:39 AM, Blogger boniphace said...

Karibu Gadiel ukumbi huu utatanuka na malipo yake utayaona siku si nyingi. Kasi uliyoanza nayo imenipa faraja na kunikumbusha sana matunda ya Ihungo. Karibu nitakutangaza kwangu ili wana kaya wakutembelee pia.

 
At 4:56 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Gadiel,
Karibu sana.Umeandika mambo ya msingi,nimesoma kidogo tu,ila nakuahidi nitarudi na kusema jambo.Karibu sana.

 
At 12:06 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Ewe jungu kuu lisilo na ukoko...karibu sana!

 
At 2:13 AM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

Gadiel, umesema ukweli..tunahitaji kusaidiana. nia yetu wote ni kwenda mbele.. ninakubali kuwa mrema alifanya kazi nzuri tena sana ya kutukuka. hakuna haja basi kumdharau japo tu hakuingia ikulu.....na naamini kabisa wizara ile ana uwezo wa kuiongoza vyema kabisa.. hii umeonyesha msisitizo kuwa siasa si uadui, wote tunapendana, nia ni moja.. kwa kweli tunahitaji kushauriana na kusaidiana. kwa faida ya wote....ndio maana hata kwenye kuunda serekali za umoja, zina msada sana kuchukua watu wenye uwezo ndani ya meli watu kama mrema, sijui sisi tutafika lini huko, lakini kwa sasa kushauriana si dhambi.

karibu sana firimbi imepigwa piga gozi!

 
At 9:23 AM, Blogger zarena kewat said...

That's what everyone likes. You have a good imagination. Great post thanks you
vimax canada

 

Post a Comment

<< Home